Utata: Kiungo huyo wa England alionekana akivuta sigara aliyopewa na kaka yake.
ARSENE Wenger wiki hii atakaa chini na Jack Wilshere kuzungumzia tabia aliyoionesha wakati wa likizo yake baada ya kombe la dunia.
Wilshere amemchukiza Wenger baada ya wiki iliyopita kupigwa picha akivuta sigara na kunywa pombe kwenye bwawa la kuogelea.
Wenger aliwahi kumkalipia Wilshere kwa
tabia yake hiyo mwezi novemba mwaka jana wakati nyota huyo mwenye miaka
22 alipopigwa picha akivuta sigara wakati wa mtoko wa usiku na alimuonya
kuwa tabia hiyo itamharibia heshima yake.
Mzee kwa kazi: Arsene Wenger kuelekea
katika mechi ya jumamosi ya maandalizi ya kabla ya msimu baina ya
Arsenal na Boreham Wood.
Sasa kocha wa Asernal atakaa na kiungo huyo akiwa kambini Amerika-lakini amesisitiza kuwa matendo hayo hayamhusu sana.
"Sijazungumza naye, kwahiyo inakuwa ngumu kwangu kusema lolote. Najua mnachoweza kufanya katika picha".
"Nataka kuzungumza naye kabla ya
kuzungumza hadharani. Tutazungumza wiki hii. Sihusiki sana na hilo,
lakini nahitaji kujua nini kilitokea".
Wilshere ameichezea Asernal chini ya Wenger kwa miaka mingi.
Amerudi kazini: Wilshere alirudi na kujiunga na maandalizi ya kabla ya msimu na hapa yupo na mchezaji mwenzake Theo Walcott.
Wenger alikiri kuwa msimu ujao unaweza kuwa mzuri au mbaya kwa Wilishere.
Alisema: "Yupo katika umri ambao
unahitaji kumuona anasonga mbele. Ni mchezaji muhimu. Namuamini, kitu
cha msingi ni maandalizi mazuri na kuwa na malengo ya kuwa fiti".
"Jack ni mchezaji mkubwa, ana akili ya mpira na malengo. Nina uhakika kama hatakuwa na majeruhi atakuwa na msimu mzuri".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni