
Anaonekana yupo vizuri: Wayne Rooney alifunga katika ushindi dhidi ya Liverpool mjini Miami.
LOUIS van Gaal ameanza kazi Manchester United na kutwaa 'ndoo' ya kombe la kimataifa la Guinness.
Jumatatu ya wiki hii Van Gaal aliifumua Liverpool mabao 3-1 katika mechi ya fainali mjini Miami nchini Marekani.
Mholanzi huyo anajua wazi kuwa ushindi
dhidi ya Liverpool kule Marekani umempa pointi chache kwa mashabiki,
lakini una maana kwake na ni kipimo kizuri.
Hata hivyo kocha aliyemshinda kwenye
uwanja wa Sun Life anaamini kuwa bado bosi huyo wa Man United anatakiwa
kuamka wakati wa msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England utakapoanza
agosti 16 mwaka huu.
Brendan Rodgers alionya kuwa Van Gaal
asitarajie urahisi katika soka la Uingereza na kutumia uzoefu aliopata
na klabu za Barcelona, Ajax na Bayern Munich, kwani katika mataifa ya
timu hizo kunakuwa na klabu moja au mbili zinazotawala.
Van Gaal ameshinda makombe matatu akiwa
na klabu tatu, yaani Hispania, Uholanzi na Ujerumani. Lakini Rodgers
anaamini atakabiliana na upinzani mkubwa akifundisha ligi kuu England.
"Nadhani itakumbana na ushindani katika
ligi hii tofauti na ligi zingine alizowahi kufanya kazi,' Alisema Bosi
wa Liverpool. "Ligi nyingi kuna timu moja au mbili tu na huwa
zinatarajiwa kushinda ubingwa".

Kombe la kwanza: Darren Fletcher na Rooney wakishangilia baada ya kutwaa kombe la kwanza chini ya Louis Van Gaal
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni