Hakuna presha: Jose Mourinho ameweka wazi kuwa atakabiliana na ugumu kuwania ubingwa msimu huu.
JOSE Mourinho amedai kuwa kama timu yake
itaishia nafasi ya pili atakuwa hajashindwa licha ya kupewa nafasi ya
kutwaa ubingwa na ikiwa imetumia paundi milioni 75 mpaka sasa katika
soka la usajili.
Mourinho alimuita Arsene Wenger 'Bingwa
wa kushindwa' akirejea ukame wa miaka 9 bila kikombe ingawa ulimalizwa
mwezi mei mwaka huu baada ya kushinda kombe la FA.
Mreno huyo amewapunguzia presha
wachezaji wake kwa kusema: "Hii ni ligi pekee duniani ambayo timu nne,
tano au sita zinashindania ubingwa. Moja tu inaweza kushinda. Unaweza
kusema nyingine zimeshindwa? sidhani.
Ufunguzi wa msimu: Mwalimu wa kireno, Jose Mourinho anajiandaa na mechi ya ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Burnley kesho.
"Jambo moja ni kwamba timu moja
inafanikiwa na tano zinashindwa. Jambo jingine ni kwamba timu tatu, nne
au tano zinaonesha kiwango cha juu, lakini moja inashinda".
Chelsea wataanza msimu huu katika dimba la Turf Moor dhidi ya Burnley kesho jumatatu na Mourinho aliongeza:
"Siwezi kufanya lolote zaidi ya kusema:
"Tunajiona washindani wa ubingwa." Kitu pekee ninachoweza kuongeza ni
kwamba, kama unamuuliza kila meneja wa ligi kuu, wewe ni mshindani wa
ubingwa?, labda wanne, watano au sita wanaweza kujibu, "Ndiyo'
Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich na bodi ya Stamford Bridge inatarajia kuona Mourinho anashindania ubingwa.
Lakini wanaelewa kuwa ushindani umeongezeka na wamekubali kuwa kushinda kombe ni jambo gumu zaidi ya huko nyuma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni