Diego Costa aliifungia Chelsea bao la kuongoza dhidi ya timu ngumu ya Leicester.
JOSE Mourinho aliwajia juu wachezaji
wake kuwa ni wavivu kufuatia kucheza vibaya kipindi cha kwanza licha ya
ushindi wa mabao 2-0 waliopata jana dhidi ya Leicester.
Chelsea walibanwa mbavu kipindi cha kwanza na timu mpya iliyopanda daraja ya Leicester kabla ya Mourinho kuwawashia moto wachezaji wake wakati wa mapumziko.
Mabao ya Diego Costa na Eden Hazard yalitosha kuwapa ushindi The Blues katika dimba la Stamford Bridge.
Vijana kazeni: Jose Mourinho aliwajia juu wachezaji wake baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Mourinho hakafurahishwa na mwanzo wa taratibu.
Alisema: "Napenda kufanya mazoezi
asubuhi, lakini wiki hii nilifanya mazoezi mchana kwasababu sio hali
nzuri ya kucheza mpira, unapata uvivu".
"Kipindi cha kwanza timu ilicheza kivivu na sikupenda kabisa.
"Lakini walijiboresha kipindi cha pili na kushinda, hiki ndicho kitu muhimu zaidi"
"Wakati wa mapumziko tuliwakalipia
kidogo. Niliwaambia kuwa jinsi tunavyocheza haitoshi kushinda mchezo na
walikuwa katika hatari"
Shangwe: Baada ya Chelsea kufunga mabao mawili, furaha ilitawala.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni