Angel Di Maria aliichezea Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid katika mechi ya Super Cup
MANCHESTER United wanakaribia kukamilisha usajili ghali wa Muargentina, Angel Di Maria kwa paundi milioni 60.
Uhamisho huo ukikamilika utavunja rekodi ya klabu hiyo katika usajili.
United wamekuwa wakifuatilia dili la
nyota huyo wa Real Madrid kwa muda mrefu na inafahamika kuwa wametoa ofa
ya mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki.
Kiwango cha juu: Di Maria anatarajia
kujiunga na Manchester United kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 60
na mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki.
Kifaa cha ukweli: Gary Neville anaamini kuwa Di Maria ndio aina ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa na Manchester United
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni