Kocha mkuu wa Yanga sc (katikati), Mbrazil Marcio Maximo amewasili kisiwani Unguja kuendelea kuiwinda ligi kuu Tanzania bara
BAADA
ya kukamilisha programu ya mazoezi ya siku tano kisiwani Pemba, kikosi cha
Yanga kimewasili kisiwani Unguja (Zanzibar) tayari kwa kumalizia siku nyingine tano
zilizosalia.
Yanga
imeweka kambi ya siku 10 Zanzibar na tayari imekata tano ikiwa pemba ambapo
ilicheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Chipukizi FC katika uwanja wa Gombani
na kushinda bao 1-0.
Bao
hilo pekee lilifungwa na mshambuliaji Mbrazil Geilson Santos Santos Santana ‘Jaja’
katika dakika ya 6 ya mchezo.
Katika
mechi hiyo iliyokuwa ya kwanza kwa kocha mkuu, Mbrazil Marcio Maximo, Yanga
ilitumia vikosi viwili tofauti kwa kila kipindi.
Ikiwa
kisiwani Unguja, kesho Yanga inatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya
Shangani FC majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa Aman mjini Zanzibar.
Hii
itakuwa mechi nyingine muhimu kwa Maximo kuona kama wachezaji wake wamefuta
makosa ya mechi ya Gombani au hapana, ili ajue nini cha kufanya zaidi kabla ya
kuanza kwa msimu mpya wa ligi septemba 20 mwaka huu.
Wakati
huo huo Mahasimu wao, Simba chini ya kocha Patrick Phiri wapo mjini Unguja
wakiendelea na mazoezi yao.
Leo
Simba walifanya mazoezi kidogo ili kuiandaa miili ya wachezaji kwa ajili ya
mechi ya kwanza ya kirafiki kesho uwanja wa Aman dhidi ya Kilimani FC.
Kocha mkuu wa Simba akiongea na wachezaji wake
Mechi hii itapigwa majira ya 2:00 usiku saa chache tu kupita baada ya kuishuhudia Yanga ikicheze katika uwanja huo huo.
Mechi hii itapigwa majira ya 2:00 usiku saa chache tu kupita baada ya kuishuhudia Yanga ikicheze katika uwanja huo huo.
Mechi
hizo zitatoa burudani kwa mashabiki wa Yanga na Simba visiwani Zanzibar
kwasababu watazishuhudia timu zao zikicheza uwanja mmoja kwa kupishana saa
chache.
Kocha
wa Simba kwa muda mrefu sasa amekuwa akiwafundisha vijana wake jinsi ya
kumiliki mpira, kukaba kwa mipango na kushambulia kwa kasi.
Lengo
la Phiri ni kuifanya Simba kuwa bora katika maeneo hayo matatu kabla ya kuanza
ligi kuu.
Simba
wataanza kucheza mechi nyingi nyumbani ambapo mechi ya ufunguzi Septemba 21
uwanja wa Taifa watachuana na Wagosi wa Kaya, Coastal Union ambao nao wako
Pemba kujifua.
Yanga wao wataanza kampeni ya kusaka ubingwa septemba 20 katika dimba la Jamhuri mkoani Morogoro dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni