Usajili: Radamel Falcao alijiunga na
Monaco majira ya kiangazi mwaka jana baada ya kucheza kwa mafanikio
katika klabu ya Atletico Madrid.
RADAMEL Falcao bado anazivutia klabu za
England ikiwemo Liverpool, ingawa mchezaji mwenyeye ana matumaini ya
kujiunga na Real Madrid.
Mshambuliaji huyu wa Colombia, ambaye
mwaka jana alijiunga na Monaco ya Ufaransa kwa dau la paundi milioni 50
kutokea klabu ya Atletico Madrid anaonekana kutoridhishwa na ligi ya
Ufaransa na anatamani kurudi Madrid.
Majira haya ya kiangazi tayari Real Madrid wametumia paundi milioni 90 kuwasajili James Rodriguez, Toni Kroos na Keylor Navas na sasa wanajipanga kutovunja sheria ya matumizi ya fedha ya UEFA.
Liverpool wanataka kumchukua Falcao kwa
mkopo kwa malengo ya kumsajili moja kwa moja msimu ujao, lakini Monaco
hawataweza kukubaliana na masharti hayo wakati wanaamini Real Madrid
wataweza kulipa dau zuri.
La Liga: Real Madrid wanaiwania saini ya Radamel Falcao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni