Louis van Gaal akitoka uwanjani baada ya kipigo cha Manchester United.
LOUIS van Gaal amekiri kuwa kujiamini
kwa Manchester United kumepunguzwa na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa
Swansea City katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu England jana uwanja
wa Old Trafford.
Bao la dakika ya 72 la Gylfi
Sigurdsson liliharibu rekodi ya kushinda mechi sita mfululizo katika
maandalizi ya msimu na United kufungwa kwa mara ya kwanza katika mchezo
wa ufunguzi ndani ya dimba la OT kwa miaka 42.
"Unaposhinda kila kitu wakati wa
maandalizi na unapoteza mechi ya kwanza, haiwezi kuwa mbaya sana,'
alisema. "Tumejenga kujiamini sana na inaweza kupunguzwa kwasababu ya
matokeo haya".
Mambo magumu: Ryan Giggs na Van Gaal wakionekana kukata tamaa baada ya kipigo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni