KLABU ya Liverpool
imemtengea ofa ya mkataba wa mwaka mmoja mshambuliaji wa zamani wa
Chelsea Samuel Eto’o ili aweze kutua Anfield.
Liverpool ambao
wanakaribia kumsajili Mario Balotelli kutoka AC Milan, pia wako tayari
kumleta na Eto’o wakati meneja Brendan Rodgers akiwa katika mipango ya
kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kabla ya kufungwa kwa dirisha la
usajili.
Eto’o ni mchezaji huru toka alipoondoka Chelsea mapema kiangazi
na amekuwa akivivutia vilabu kadhaa barani Ulaya, Amerika na Mashariki
ya Kati. Ila nyota huyo wa kimataifa wa Cameroon bado anataka kubakia
nchini Uingereza baada ya kucheza kwa mafanikio msimu mmoja akiwa na
Chelsea. Vilabu vya Ajax Amsterdam ya Uholanzi na Everton vimeonyesha
nia ya kumtaka lakini inaonekana Liverpool sasa ndio wako katika nafasi
nzuri ya kumchukua nyota huyo wa zamani wa Barcelona na Inter Milan.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni