MENEJA wa klabu ya
Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa anaona tofauti anapomuona Cesc
Fabregas akiichezea Chelsea katika fulana ya bluu lakini amesisitiza
kuwa hajutii kutomsajili tena.
Wenger aliwaambia waandishi wa habari
kuwa kitu pekee anachojutia ni kuondoka kwa Fabregas mwaka 2011 kwenda
Barcelona na kudokeza kuwa bado anataka kusajili kiungo mwingine kabla
ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania
mwenye umri wa miaka 27 ambaye amecheza mechi zaidi ya 300 akiwa
Arsenal alianza vyema katika timu yake mpya ya Chelsea wakati
waliposhinda mabao 3-1 dhidi ya Burnley Jumatatu. Wenger amesema hajutii
mchezaji huyo kujiunga na mahasimu wao ingawa anaona tofauti lakini
inabidi ukubali kuwa ni kawaida kwa wachezaji wa kulipwa kuhama kutoka
klabu moja kwenda nyingine. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kuondoka
kwa Fabregas kulimpa nafasi nyota wa kimataifa wa Wales Aaron Ramsey
mwenye umri wa miaka 23 kuibuka katika kikosi chake kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni