STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 22 Agosti 2014

NEYMAR AUMIA TENA.

KLABU ya Barcelona imepata pigo kubwa kuelekea katika mchezo wao wa ufunguzi wa La Liga dhidi ya Elche utakaochezwa Jumapili kutokana na taarifa za kukosekana kwa Neymar katika mchezo huo wa Camp Nou kutokana na majeruhi. 
 
Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, ndio kwanza alikuwa ameruhusiwa kucheza na madaktari wa timu hiyo baada ya kupona majeruhi ya mgongo aliyopata katika Kombe la Dunia lakini sasa anakabiliwa na majeruhi mengine. 
 
Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, imedai kuwa Neymar alikuwa akilalamika maumivu katika kifundo chake cha mguu wa kushoto na baada ya vipimo imegundulika kuwa ana matatizo ambayo yatachukua muda kidogo kupona. Taarifa hiyo imeendelea kudai kuwa kurejea mazoezini kwa mchezaji huyo kutategemea kumalizika kwa maumivu hayo hivyo ni wazi hatakuwepo katika mchezo wa kesho. Neymar alicheza mechi 26 za La Liga msimu uliopita na kufunga mabao saba lakini msimu huu unaonekana tayari ameuanza vibaya kwa maumivu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox