Msafara wa watu 35 ukiwa na wachezaji 27 na benchi
la Ufundi 8 wa timu ya Young Africans tayari umeshawasili Kisiwani Pemba kwa
ajili ya maandalizi ya mwisho kujiandaa na mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom
msimu wa 2014/2015.
Kocha mkuuu Marcio
Maximo na kikosi chake wamefikia katika hoteli ya kitalii ya Pemba Misali
iliyopo eneo la Wesha na watakua wakijifua kwa muda wa takribani siku 10 kabla
ya kurejea jijini Dar es salaam mwisho wa mwezi huu.
Kikosi cha Young
Africans kitakua kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani mjini Chake Chake
na siku ya alhamis wanataraji kucheza wa kwanza wa kirafiki dhidi ya timu ya
Chipukizi ya kisiwani Pemba.
Kulingana na program
ya bench la Ufundi kisiwani Pemba, Young Africans inatarajia kucheza michezo
mitatu ya kirafiki na timu za kutoka Visiwa vya Pemba na Unguja na baadae
kurejea Dar es salaam kwa michezo mwili ya kimataifa kabla ya kucheza mchezo wa
Ngao ya Hisani septemba 13, 2014.
Wachezaji waliondoka
kuelekea Pemba ni:
Walinda Mlango:
Juma Kaseja, Ally
Musatfa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida"
Walinzi wa Pembeni:
Juma Abdul, Salum
Telea, Oscar Joshua, Edwad Charles na Amos Abel
Walinzi wa Kati:
Kelvin Yondani, Nadir
Haroub "Cannavaro", Rajab Zahir na Pato Ngonyani.
Viungo:
Mbuyu Twite, Said
Juma "Makapu", Omega Seme, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima na Hamis
Thabit.
Viungo wa Pembeni:
Saimon Msuva, Mrisho
Ngasa, Nizar Khalfani na Andrey Coutinho.
Washambuliaji:
Geilson Santos
"Jaja", Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Hamis Kizza na Hussein
Javu
Benchi la Ufundi
walioko Kisiwani Pemba ni:
Kocha Mkuu : Marcio Maximo
Kocha wasaidizi Leonado Neiva, Salvatory Edward
Kocha wa Makipa: Juma Pondamali
Daktari wa timu: Dr Suphian Juma
Meneja wa timu:
Hafidh Saleh
Mchua Misuli: Jaco Onyango
Mtunza Vifaa: Mahmod Omar
"Mpogolo"
Chanzo: Tovuti ya Yanga sc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni