MENEJA wa Real Madrid,
Carlo Ancelotti amedai hajawahi kufananisha mafanikio yake katika klabu
hiyo na ya kocha Jose Mourinho. Kocha huyo wa zamani wa Paris
Saint-Germain alichukua nafasi ya Mourinho mwaka 2013 baada ya kocha
huyo kuisaidia timu hiyo kushinda taji la La Liga, Kombe la Mfalme na
Kombe la ligi katika miaka mitatu aliyokuwepo Santiago Bernabeu. Hata
hivyo, inadaiwa aliondoka katika klabu hiyo kwa utata kufuatia taarifa
za kutoelewana na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na kushindwa
kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ancelotti alionekana kufikia
mafanikio hayo katika msimu wake wa kwanza kwa kuwafunga mahasimu wao
Atletico Madrid katika mchezo wa fainali huku
pia
akishinda Kombe la Mfalme na Kombe la Ligi. Matokeo hayo yanafanya
wawili hao kulinganishwa mafanikio yao katika timu hiyo lakini Ancelotti
amejitoa katika ulinganyisho huo na kudai kuwa yeye anajaribu kufanya
kazi yake kila siku katika ubora. Ancelotti amesema hajawahi
kulinganisha mafanikio yake na Mourinho katika klabu hiyo kwnai ana
mambo mengi ya kufikiria huku akijaribu kuisaidia timu hiyo iweze
kufanya vyema zaidi.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni