HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa dakika chache zilizopita ni kwamba klabu ya Yanga imemsajili mshambuliaji wa Simba aliyeachwa Amisi Tambwe .
Yanga imemsajili Tambwe dakika chache zilizopita ambapo anakuja kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Emerson Oliveira wa Brazil aliyetemwa kwa kukosa ITC.
Tambwe ametua Yanga ikiwa ni siku chache baada ya Mganda Hamis Kiiza kuachwa na klabu hiyo na kukimbilia URA ya Uganda baada ya Kpeh Seen Sherman wa Liberia kupewa kandarasi ya kuichezea timu hiyo.
Tambwe alikuwa mfungaji bora wa ligi msimu uliopita ambapo alifunga mabao 19 kwenye ligi lakini alishindwa kuwika msimu huu baada ya kutopewa nafasi ya kutosha chini ya Patrick Phiri.
Simba imemuacha Tambwe baada ya kumsajili Danny Serunkuma toka Gor Mahia ya nchini Kenya .
Yanga imekamilisha usajili huu saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa leo na TFF
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni