Kocha Hans van Der Pluijm ametua jijini Dar
es Salaam, tayari kuchukua nafasi ya Marcio Maximo.
Pluijm amewasili usiku wa kuamkia leo,
lakini akakataa katakata kuweka wazi kwamba yuko tayari kuchukua nafasi hiyo.
Badala yake, Pluijm amesema amekuja nchini
kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga.
“Ngoja nifanye mazungumza na uongozi wa
Yanga, halafu tutaongea,” alisema.
Pluijm aliondoka Yanga kwenda Al Shaolah FC ya Saudi Arabia ambayo ilimzingua, akaamua kubwaga manyanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni