Marcio Maximo na msaidizi wake Leonardo Neiva wakati wakiinoa Yanga |
KAMA ilivyokuwa kwa kocha Ernie Brandts aliyetimuliwa baada ya Yanga kufungwa na Simba kwenye mchezo wa 'bonanza' wa Nani Mtani Jembe, hali hiyo imemkuta Marcio Maximo.
Kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars kutoka Brazil ametimuliwa Yanga baada ya kipigo cha mabao 2-0 katika pambano la Nani Mtani Jembe-2.
Taarifa ambazo ni za uhakika toka ndani ya Yanga zinasema kuwa, kocha Maximo amepewa mkono wa kwaheri na nafasi yake inarudi kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Hans Van Der Pluijm.
Mmoja wa viongozi wa kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga amesema, Maximo ataondoka nchini ndani ya siku tatu baada ya kukubaliana na uongozi.
"Si kwamba amefukuzwa, lakini ni makubaliano kwamba anaondoka.
"Ni kweli, lakini msitake kulikuza hili jambo ionekane kama tumemfukuza," aliuliza na alipotakiwa kujua mrithi ni nani, alikataa kusema.
Hata hivyo ni kwamba Maximo amepewa mkono wa KWAHERI sambamba na kiungo aliyekuja naye toka kwao, Emerson Oliveira ambaye inaelezwa amekosa ITC japo ukweli ni kwamba ameonekana ni bomu.
Yanga ilimfurusha Brandt na wasaidizi wake, Fred Felix Minziro na Razack Ssiwa baada ya timu yao kulala mabao 3-1 na safari hii Maximo anaondoka na wasaidizi wake akiwamo Mbrazil mwenzake Leonardo Neiva ambaye alimleta baada ya kusaini mkataba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni