Kulaaa! Neymar akimlamba kichwa beki wa Valencia aliyemchezea kitemi kabla |
Mzozo baina ya wachezaji wa Valencia na Barcelona |
Barcelona walioivaa Valencia katika uwanja wa Mestalla walipata ushindi huo kupitia bao la 'jioni' lililofungwa na Sergio Busquets dakika ya 90, kabla ya Lionel Messi kupigwa na chupa. Katika pambano hilo lilishuhudiwa undava ukitembezwa uwanjani kwatai Neymar alipompiga kichwa Nicolas Otamendi baada ya beki huyo kuanza kumcheza ‘kitemi’ Mbrazil huyo. Otamendi alimchezea kibabe Neymar kwenye eneo la hatari, lakini alipokwenda kumuinamia kumuomba msamaha, alilambwa kichwa ‘kishikaji’ kabla ya kuibuka mzozo uliohusisha wachezaji wote.
Hata hivyo Neymar hakuchukuliwa hatua zozote na refa wa pambano hilo, David Fernandez.
Ushindi huo umeifanya Barcelona kufikisha pointi 31, mbili nyuma ya Real Madrid wanaoongoza msimamo ambao walishinda mabao 2-1 ugenini siku ya Jumamosi dhidi ya Malaga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni