STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 29 Desemba 2014

BREAKING NEWZZZZZZ... PATRIC PHIRI ATIMULIWA SIMBA ... KOCHA MPYA KUTUA NCHINI KESHO




Patric Phiri

Kocha Patrick Phiri amesema ametaarifiwa kuhusiana na kibarua chake kusitishwa.



Phiri raia wa Zambia amesema ni suala la kawaida kumtokea kocha, hivyo hana kinyongo na uongozi wa klabu hiyo.

"Wamenitaarifu kuhusiana na kuachishwa kazi, hili si jambo jipya, ingawa niliona tungeweza kubadilisha mambo.

"Najua Simba wanataka kufanya vizuri, hivyo siwezi kumlaumu mtu na utaona mwendo wa timu yetu ulivyokuwa," alisema Phiri.

Phiri amesema anasubiri kiasi cha fedha alichokuwa anadai ambacho hakueleza ni kiasi gani, halafu ataanza safari ya kurejea kwao Zambia.

"Nikimalizana nao kuhusiana na malipo yangu, nitajua lini ninakwenda nyumbani," alisema Phiri.

 Anayetarajiwa kuwa kocha mpya wa Simba Goran Kopunovic, anataraji kuwasili nchini kesho jumatano

Mrithi wa Phiri ni Mserbia Goran Kopunovic ambaye atasaidiwa na Jean Marie Ntagawabila kutoka nchini Rwanda kwa maana hiyo kibarua cha Suleiman Matola pia kipo shakani.

Kopunovic aliwahi kufanya kazi kwa mafanikio akiwa na klabu ya Polisi nchini Rwanda kwa miaka mitatu kabla ya kutimkia nchini Vietnam ambapo pia alifanya kazi kwa mafanikio pia.

Kocha huyo ambaye ni muumini wa soka la kuvutia na kuburudisha pia anasifika kwa mazoezi magumu ili wachezaji wake na nguvu na kasi ya ajabu.

Kumbuka kocha anayeondoka Patric Phiri tangu ajiunge na Simba kwa mara ya tatu mwezi agost mwaka huu ameiongoza timu hiyo kwenye michezo 22, akishinda michezo nane kati ya hizo ni ushindi mmoja tu ndio ameupata kwenye ligi kuu ya VPL walipoifunga Ruvu Shooting 1-0 na ushindi wake wa mwisho na Simba ni ule alipoifunga Yanga 2-0 kwenye mchezo wa Nani mtani jembe.



 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox