Simba imemaliza mechi yake ya kirafiki dhidi ya
Express ya Uganda kwa sare ya bila kufungana.
Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar, leo ilikuwa ya kuvutia huku kila upande ukishambulia kwa nguvu.
Pamoja na juhudi za Simba kutaka kushinda
lakini Waganda hao walionekana kucheza soka la kujiamini na walikuwa watulivu
zaidi.
Kila upande utajilaumu kwa kupoteza nafasi ya kupata mabao ya ushindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni