Mwenyekiti wa Kamati ya Uteandaji ya Simba SC, Zacharia Hanspope amethibitisha muda mfupi uliopita juu ya usajili huo na kuweka wazi kwamba wameamua kumwongeza kandarasi hiyo nyota huyo baada ya kuona mchango wake katika kikosi chao.
“Okwi ni mchezaji mzuri, amekuwa akifanya kazi nzuri katika kikosi chetu. Leo tumemuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja,” amesema Hanspope.

Okwi aliyezaliwa Desemba 25, 1992, amesaini mkataba huo mbele ya Rais wa Simba SC, Evans Aveva.
Okwi alijiunga na Simba SC kwa mkataba mfupi wa miezi sita Agosti mwaka huu ili kulinda kiwango chake wakati akiendelea na kesi iliyokuwa ikimkabili dhidi ya Yanga SC. Mganda huyo alishinda kesi hiyo baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuthibitisha kwamba mkataba wake na Yanga SC ulikuwa umevunjwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni