MSHAMBULIAJI
Thierry Henry ametangaza kuondoka klabu ya New York Red Bulls ya
Marekani baada ya kuitumikia kwa miaka minne na nusu katika Ligi Kuu ya
nchini humo.
Mwanasoka
huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, ametangaza uamuzi wake huo
siku tatu baada ya kukiri anapenda kurudi Arsenal, na kubadilisha picha
yake ya bango katika ukurasa wake wa Facebook kwa kuweka picha ya Uwanja
wa Emirates.
Mkongwe
huyo mwenye umri wa miaka 37 atatumia wiki chache zijazo kuamua
mustakabali wake wa baadaye wa maisha, huku kufundisha klabu katika Ligi
Kuu ya England ikiwa moja ya mipango.
Thierry Henry, pichani akishangilia bao Januari mwaka 2012, amesema angependa kurejea Arsenal
MATAJI YA THIERRY HENRY NA KLABU ALIZOCHEZEA
1994-1999: Monaco (Mechi 105, mabao 20)
1999-1999: Juventus (Mechi 16, mabao 3)
1999-2007: Arsenal (Mechi 254, mabao 174)
2007-2010: Barcelona (Mechi 80, mabao 35)
2010-2014: New York Red Bulls (Mechi 122, mabao 51)
2012-2012: Arsenal (mkopo) (Mechi 4, bao 1)
1997-2010: Ufaransa (Mechi 123, mabao 51)
Monaco: Ligue 1, Taji la ubingwa
Arsenal: Ligi Kuu (2), Kombe la FA (3), Ngao ya Jamii (2)
Barcelona: La Liga (2), Kombe la Mfalme, Super Cup ya Hispania, Ligi ya Mabingwa, Super Cup ya Ulaya, Klabu Bingwa ya Dunia
New York Red Bulls: MLS Kanda ya Mashariki (2), Ngao ya Mashabiki
Ufaransa: 1998 Kombe la Dunia, Euro 2000, Kombe la Mabara 2003
Henry amebadilisha picha yake ya bango Facebook na kuweka ya Uwanja wa Emirates
"Nachukua fursa hii kutangaza kwamba kwa bahati mbaya Jumamosi ilikuwa mechi yangu ya mwisho kwa New York Red Bulls," Henry amesema leo.
Henry aliliambia jarida la L'Equipe la Ufaransa Ijumaa kwamba atabakia kwenye soka baada ya kustaafu kama mchezaji kwa kugeukia ukocha, ushauri au utendaji.
Mshindi
huyo wa Kombe la Dunia mwaka 1998 amekiri kujuta kushindwa kuisaidia
Arsenal kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na ndiyo maana anataka
kwenda kutoa mchango wake katika klabu ipate mafanikio Ulaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni