MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Mashabiki jana.
Mpachika
mabao huyo wa mabingwa wa Ligi Kuu ya England na washindi wa pili wa
Kombe la Dunia, Argentina, alishinda tuzo hiyo katika hoteli ya St
Pancras Renaissance mjini London, England.
Sergio Aguero akiwa na tuzo yake kwa pamoja na mpenzi wake, Karina Tejeda
Nahodha
wa Manchester United na England, Wayne Rooney na winga wa Real Madrid
na Wales, Gareth Bale pia walikuwemo kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo
sambamba na nyota wengine wa Ligi Kuu England, Thibaut Courtois,
Branislav Ivanovic, Vincent Kompany, Pablo Zabaleta, Angel di Maria,
Cesc Fabregas, Eden Hazard, Mesut Ozil, Yaya Toure, Sergio Aguero na
Diego Costa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni