Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Manuel Neuer ndiyo
vichwa vitatu vilivyoteuliwa kuwania tuzo ya FIFA Ballon d'Or 2014.
Watatu hao ndiyo wameingia fainali na mshindi
atapatikana Januari 12, 2015.
Neuer, 28, aliteuliwa mara ya mwisho mwaka 2006
kuwania tuzo hiyo, usisahau ndiye aliiwezesha Ujerumani kubeba Kombe la Dunia
Brazil mwaka huu.
Messi, ndiye mchezaji anaongoza kwa kutwaa tuzo nyingi
kama hizo, amebeba mara nne na kwa jina la Ballon d'Or ni kwa miaka hii (2009-2012).
Cristiano Ronaldo anapambana kupata tuzo yake ya tatu Ballon
d'Or.
Alitwaa ya kwanza mwaka 2008 akiwa na Manchester United na mara ya mwisho akiwa na Real Madrid na ndiye mtetezi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni