MENEJA wa klabu ya
Manchester United, Louis van Gaal ameonyesha kutofurahishwa na ratiba ya
Ligi Kuu itakavyokuwa katika kipindi cha sikukuu za krismasi na mwaka
mpya. Kuna uwezekano mkubwa United ikacheza mechi nne ndani ya siku tisa
katika kipindi cha kati ya Desemba 29 mpaka Januari 3 kutegemeana na
ratiba ya Kombe la FA itakavyokuwa. Ratiba katika Ligi Kuu inaonyesha
kuwa watakuwa wenyeji wa Newcastle United Desemba 26, kabla ya kucheza
wa ugenini dhidi ya tottenham Hotspurs siku mbili baadae na siku ya
mwaka mpya watapepetana na Stoke City. Akihojiwa Van Gaal amesema ana
mke, watoto na wajukuu na hawezi kuwaona katika kipindi cha krismasi
lakini alitaka kufanya kazi katika Ligi Kuu hivyo anapaswa kuzoea hali
iliyopo. Van Gaal amesema hafurahishwi na suala hilo lakini hawezi
kubadilisha na hadhani kama ni jambo zuri kwa wachezaji pia.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumatatu, 1 Desemba 2014
VAN GAAL ACHUKIZWA NA RATIBA YA LIGI KUU KIPINDI CHA KRISMASI.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni