Kikosi
cha Taifa Stars Maboresho kimeingia kambini leo (Desemba 1 mwaka huu)
Bulyanhulu mkoani Shinyanga kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya
Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ikiwa
chini ya Kocha Mart Nooij, Stars Maboresho itapiga kambi mkoani humo
hadi Desemba 6 mwaka huu ambapo itarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa
ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa.
Wachezaji
walioingia kambini ni Abubakar Ally (Coastal Union), Abubakar Ally
Mohamed (White Bird), Aishi Manula (Azam), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar),
Atupele Green (Kagera Sugar), Edward Charles (Yanga) na Emmanuel
Semwanda (African Lyon).
Gadiel
Michael (Azam), Hashim Magoma (Stand United), Hassan Banda (Simba),
Hassan Mwasapili (Mbeya City), Joram Mgeveke (Simba), Kassim Mohamed
Simbaulanga (African Lyon), Kelvin Friday (Azam) na Makarani Ally
(Mtibwa Sugar).
Miraji
Adam (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar),
Omari Nyenje (Ndanda), Pato Ngonyani (Yanga), Rashid Mandawa (Kagera
Sugar), Said Hamisi (Simba), Salim Hassan Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shiza
Ramadhan (Mtibwa Sugar).
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaishukuru kampuni ya kuchimba
madini ya Acacia Mining PLC (zamani African Barrick Gold PLC) kwa
kufadhili kambi ya Stars kupitia mgodi wa Bulyanhulu.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni