MENEJA wa klabu ya
Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa hakuna mchezaji yeyote katika Ligi
Kuu aliyezoea mazingira haraka kuliko Alexis Sanchez. Mshambuliaji huyo
wa kimataifa wa Chile ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Barcelona
Julai amefunga bao lake la tisa kwa msimu huu jana wakati rsenal
ikiibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Southampton. Wenger
amesema ni vigumu kutafuta mfano wa mchezaji aliyezoea haraka mazingira
kama ilivyo kwa Sanchez kwani amekuwa na uchu wa ushindi. Sanchez sasa
anakuwa amefunga mabao 14 katika mechi 22 za mashindano yote
alizoichezea Arsenal toka ajiunge nao akitokea Camp Nou kwa kitita cha
paundi milioni 35. Akiwa Barcelona Sanchez aliifungia mabao 47 katika
mechi 141 huku akiifungia nchi yake mabao mawili katika michuano ya
Kombe la Dunia iliyofanyika Brazil majira ya kiangazi.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Alhamisi, 4 Desemba 2014
WENGER AMMWAGIA MISIFA KEMKEM SANCHEZ BAADA YA KUOKOA JAHAZI JANA.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni