KATIKA kipindi hiki cha
usajili wa dirisha dogo la usajili taarifa mbalimbali zimekuwa zikivuma
huku kule kuhusiana na mchezaji huyu na yule. Mojawapo ya habari
zilizopamba vichwa vya habari vya baadhi ya magazeti hivi leo ni pamoja
na taarifa kuwa klabu ya Manchester United imepanga kuvunja kibubu na
kumrejesha kiungo Paul Pogba kutoka klabu ya Juventus. Kiungo huyo wa
kimataifa wa Ufaransa aliondoka United kuelekea Juventus mwaka 2012
lakini sasa anaweza kurejea Old Trafford baada ya kuripotiwa kuwa meneja
Louis van Gaal yuko tayari kutoa kitita cha euro milioni 90. Juventus
nao wanafikiria mchezaji atakayechukua nafasi ya mshambuliaji wao Carlos
Tevez wakati atakapoondoka. Tevez ameshaweka wazi kuwa hana mpango wa
kuongeza mkataba katika timu hiyo pindi utakapomalizika na Juventus
wanadhaniwa kuwa wanaweza kumuwinda Radamel Falcao ili kuziba nafasi
hiyo. Klabu ya Real Madrid nayo imeingia katika mbio za kumuwinda
mshambuliaji wa Swansea City Wilfried Bony. Madrid wanamtaka Bony ili
aweze kusaidiana na Karim Benzema huku Manchester City, Liverpool na
Tottenham Hotspurs nazo zikimuwinda kwa karibu nyota huyo wa kimataifa
wa Ivory Coast. Kuna taarif nyingine kutoka nchini Uingereza kuwa
mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abromovich anatarajia kujaribu
kumsajili Lionel Messi kama Barcelona haitashinda taji lolote msimu
huu. Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ametoa ombi la kusajiliwa kwa
mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina ambaye amewahi kushinda
mataji manne ya Ballon d’Or.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Ijumaa, 2 Januari 2015
Home
/
Unlabelled
/
TETESI ZA USAJILI: MAN UNITED WAMTENGEA FUNGU POGBA, MADRID NAO WAINGIA MBIO ZA KUMUWANIA BONY.
TETESI ZA USAJILI: MAN UNITED WAMTENGEA FUNGU POGBA, MADRID NAO WAINGIA MBIO ZA KUMUWANIA BONY.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni