Wenger anataka vibali vya kazi kwa wachezaji wa kigeni vifutwe
MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger anataka vibali vya kazi kwa wachezaji wa kigeni vifutwe.
Mfaransa
huyo ambaye amekiri kwamba alishindwa kumsajili Angel di Maria klabuni
hapo miaka 9 iliyopita kwasababu ya kukosa kibali cha ajira.
Amesema
mamlaka za soka za UK zifungue mipaka kwa wachezaji wote duniani, na
sio lazima kwa wale tu wanaokidhi vigezo vya kupata vibali vya kazi kama
ilivyosasa.
Arsenal wamesimama kumsaini beki wa Villarreal, Gabriel Paulista ambaye ada yake ni paundi milioni 15.
Usajili
wa beki huyo raia wa Brazil umesimama kwasababu ya kibali cha kazi na
haitakuwa rahisi kwasababu beki huyo wa kati hajawahi kucheza soka la
kimataifa.
Gabriel Paulista (kulia) anaweza kujiunga na Arsenal kama wataweza kupata kibali cha kazi
Kanuni
inasema kuwa wachezaji ambao wamecheza asilimia 75 ya mechi za mataifa
yao ndani ya nchi 70 za juu kisoka katika miaka miwili iliyopita ndio
wanastahili tu kupata vibali vya kazi.
Hii inawanyima haki wachezaji wa akademi kujiunga na timu za kwanza. Arsenal wanasema kama watashindwa kumsajili Paulista mwezi huu watakata rufaa.
Msimu
ujao kutakuwa na kanuni mpya inayosema wachezaji wenye thamani ya
paundi milioni 10 watapewa vibali vya kazi. Lakini Wenger anasema sheria
ya vibali vya kazi inatakiwa kufutwa akidai inaweza kusaidia kupata
wachezaji vijana waliokamilika.
"Lengo la ligi kuu England ni kuwa ligi bora duniani,' Amesema Wenger. "Kwahiyo lazima uweke wazi mipaka.
"Tulimvumbua
Di Maria alipokuwa na miaka 17. Tulihitaji aje hapa, lakini alienda
Ureno, kutoka Ureno akaenda Hispania. Kwanini? Kwasababu asingeweza
kupata kibali cha kazi hapa. Hii inamaanisha unaweza kumpata England
wakati ana thamani kubwa ya fedha".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni