UAMUZI wa Luis Figo
kuingia katika kinyang’anyiro cha kugombea urais wa Shirikisho la Soka
Duniani-FIFA imepokewa vyema nchini kwake Ureno pamoja na kukabiliwa na
kibarua kigumu mbele ya rais wa sasa Sepp Blatter katika uchaguzi
utakaofanyika Mei mwaka huu. Figo mwenye umri wa miaka 42 ambaye amewahi
kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia na mmoja kati ya wachezaji bora
katika kipindi chake akiwa Real Madrid na Barcelona alitangaza nia yake
hiyo Jumatano iliyopita baada ya kukamilisha vigezo
vilivyohitajika. Muda wa mwisho wa kutuma maombi utakuwa leo usiku huku
huku Figo akiwa sambamba na wagombea wengine wasiomtaka Blatter na
kutangaza nia akiwemo Prince Ali Bin Al-Hussein kutoka Jordan, Michael
van Praag kutoka Uholanzi na Jerome Champagne na David Ginola wote
kutoka Ufaransa. Rais wa Shirikisho la Soka la Ureno-FPF, Fernando Gomes
amesema jana kuwa kujitokeza kwa FIGo kugombea nafasi hiyo ni heshima
kubwa kwa soka la nchi hiyo hivyo watamuunga mkono mpaka mwisho wa
safari yake. Waziri wa michezo wa Ureno Emidio Guerreiro pia alitangaza
serikali kumuunga mkono kiungo huyo wa zamani ambaye ameliletea taifa
hilo sifa kemkem.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Ijumaa, 30 Januari 2015
URENO YAMUUNGA MKONO FIGO KWA UAMUZI WAKE.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni