Javier Balboa akishangilia moja ya mabao ya wenyeji Guinea ya Ikweta |
Polisi wakimuokoa refa baada ya wachezaji wa Tunisia kuchukizwa na penati waliopewa wenyeji dakika za jioni |
Wenyeji Guinea ya Ikweta wakishangilia ushindi wao dhidi ya Tunisia |
DR Congo wakipongezana walipowaduwaza majirani zao Congo-Brazzaville |
Ilikuwa kama Vita baina ya Congo-Brazzaville na DR Congo |
DR Congo walityoka nyuma ya mabao 2-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Congo-Brazzaville katika mchezo uliochezwa mapema kabla ya wenyeji kuwang'oa kwenye muda wa ziada mabingwa wa zamani wa Afrika Tunisia kwa mabao 2-1.
Congo-Brazzaville walianza kuwashtua majirani zao dakika 10 baada ya kuanza kwa kipindi cha pili pale Ferebory Dore alipofunga bao la kuongoza kabla ya Thievy Bifouma kuongeza la pili dakika ya 62 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa DR Congo.
Hata hivyo DR Congo hawakukata tamaa baada ya kufungwa mabao hayo mawili na badala ake kucharuka na kurejesha bao moja baada ya jingine kupitia wachezaji wake nyota, Dieumerci Mbokani aliyefunga mabao mawili katika dakika ya 65 na 90, Jeremy Bokila dakika ya 75, na Joel KImwaki aliyefunga bao la tatu dakika ya 81 na kuivusha timu yao nusu fainali tangu 1988.
Katika meechi ya pili iliyochezwa pia kwenye uwanja huo wa Bata usiku wenyeji waliwaduwaza Tunisia kwa kuwalaza mabao 2-1 wakichomoa bao dakika ya jioni na kumaliza dakika 90 kwa sare ya 1-1 kabla ya kufunga bao la ushindi kwenye muda wa nyongeza wa dakika 30.
Tunisia walianza kuandika bao lililokuwa likionekana kama limewavusha hatua ya nusu fainali kupitia kwa Ahmed Akaichi katika dakika ya 70, lakini Guinea ya Ikweta ilichomo dakika za ziada za pambano hilo kabla ya halijamalizika kupitia kwa Javier Balboa aliyefunga kwa penati, iliyozua zogo kwa wachezaji wa Tunisia kumlalamikia mwamuzi kiasi cha Polisi kuamua kuingilia kati kumuokoa mwamuzi huyo.
Dakika ya 102 Balboa tena aliwatoa kimasomaso wenyeji wa kufunga bao la pili ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuifanya Guinea ya Ikweta kufuzu kwa mara ya kwanza hatua hiyo na sasa wanasubiri mshindi kati ya Ghana na Guinea wanaocheza leo kwenye robo fainali nyingine wa michuano hiyo.
DR Congo wenyewe watasubiri kujua watacheza nani hatua ya nusu fainali kati ya Ivory Coast na Algeria ambazo zitakamilisha mechi za robo fainali usiku wa leo kwenye uwanja wa Malabo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni