Licha ya soka la sasa kuwa limerahisishwa zaidi kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya teknolojia,hapa kuna matukio mawili yameshangaza kwa wachezaji kuwakaba washambuliaji kama mchezo wa mieleka,tukio moja ni nchini Italia kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya AC Milan na Lazio ambalo liliisha kwa AC Milan kupata ushindi wa 3-1. Kilichoshangza zaidi mashabiki ni tukio la beki wa AC Milan Philippe Mexes kumkaba koo mshambuliaji wa Lazio Stefano Mauri kama vile anataka kumuua,na refa bila kupepesa macho alimpa kadi nyekundu.
Tukio la pili ni pambano kati ya Yanga na Ruvu Shooting kwenye ligi ya Tanzania bara beki wa Ruvu Shooting George Michael alimkaba Hamis Tambwe vilevile kama tukio la Mexes ila hakuna adhabu iliyotolewa na mwamuzi, Je tatizo ni marefa wetu hawako makini ama ni kukosa teknolojia ya kurudia matukio yanayotea kwenye michezo ya ligi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni