Bondia maarufu nchini, Francis Cheka amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela na Mahakama ya mkoani Morogoro.
Taarifa zinaeleza kua, Cheka amepatikana na hatia ya kushambulia kushambulia mwili baada ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake.
Pamoja na kifungo cha miaka mitatu, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakamani hiyo, Said Msuya amemhukumu Cheka kulipa faini ya Sh milioni moja baada ya kumaliza kifungo hicho.
Cheka amepatikana na hatia ya shambulio dhidi ya aliyekuwa meneja wa baa yake, Bahati Kibanda aliyemshambulia Julai 2, mwaka jana katika Ukumbi wa Vijana Social aliokuwa ameukodi kwa ajili ya kuendesha shughuki za baa zilizokuwa zinasimamiwa na Kibanda.
Kutokana na kukutwa na hatia, Cheka amekuhukumiwa kwenda jela kwa muda huo na imeedaiwa kua tayari ameshapelekwa kwenye gereza mkoani Morogoro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni