MCHEZAJI wa zamani wa
Barcelona, Eric Abidal amesema Lionel Messi sio mashine lakini atabakia
kuwa mchezaji wa kipekee. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa alicheza
kwa kipindi cha miaka sita Camp Nou na nyota huyo wa Argentina kabla ya
kutimkia Monaco mwaka 2013. Ingawa ameshindwa kunyakuwa tuzo mbili za
Ballon d’Or zilizopita, Messi amekuwa katika kiwango bora toka kuanza
kwa mwaka huu na Barcelona imepunguza pengo la alama mpaka kufikia moja
nyuma ya vinara wa La Liga Real Madrid wakiwa wameshinda mechi 10
mfululizo. Abidal amesema Messi yuko katika kiwango chake kwa asilimia
mia moja jambo ambalo lilikuwa likitegemewa na wengi mwaka huu. Abidal
aliendelea kudai kuwa wachezaji wakubwa wataendelea kuwa wakubwa lakini
sio mashine na hiyo inakwenda hata kwa Messi lakini akiwa katika kiwango
chake cha juu kila kitu kinakwenda sawa kwa Barcelona.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Ijumaa, 13 Februari 2015
ABIDAL ADAI MESSI SIO MASHINE ILA ANA KIPAJI CHA KIPEKEE.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni