MSHAMBULIAJI wa Chelsea,
Diego Costa amedai kuwa mchezo wake ni wa kutumia nguvu lakini wa
kawaida na hajawahi kumuumiza vibaya mchezaji yeyote wa timu
pinzani. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania na mzaliwa na Brazil mwenye
umri wa miaka 26, anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu kwa
kumkanyaga Emre Can wa Liverpool katika mchezo wao wa nusu fainali ya
Kombe la Ligi mwezi uliopita. Akihojiwa Costa amesema huwa anapenda
kutumia nguvu akiwa mchezoni lakini kamwe hajawahi kumuumiza mchezaji
yeyote vibaya. Meneja wa Chelsea Jose Mourinho naye pia amemtetea Costa
na kudai alimkanyaga Can kwa bahati mbaya na sio makusudi kama wengi
wanavyodai.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Ijumaa, 13 Februari 2015
SINA HISTORIA YA KUMUUMIZA MCHEZAJI YEYOTE KWA MAKUSUDI - COSTA.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni