Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limeitaka klabu ya SC Villa ya Uganda kutolea ufafanuzi sakata la uhamisho wa mshambuliaji Emanuel Okwi
FIFA ina dukuduku juu ya kumbukumbu za uhamisho wa Okwi ambazo zimekua na utata mwingi tangu alipohamia klabu za Simba, Yanga za Tanzania na Etoile du Sahel ya Tunisia.
FIFA inatambua kwamba, wakati Okwi anahama kutoka klabu moja kwenda nyingine na pesa pia zilikua zinalipwa kwa klabu ambayo Okwi alikua anaihama. Lakini takwimu za SC Villa zinaonesha kwamba Okwi alihama kutoka SC Villa kwenda SC Villa kitu ambacho si cha kawaida.
Mkurugenzi mpya wa SC Villa, Ben Misagga aliteua kamati ya kuchunguza maswala ya uhamisho wa wachezaji wa klabu hiyo kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 ili kuchunguza sakata hilo.
Okwi alihama kutoka klabu ya SC Villa kwenda klabu ya Simba SC mwaka 2010 kabla ya kuhamia klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia mwaka 2013.
Lakini akarudi tena kwenye klabu yake ya zamani ya klabu ya SC Villa mwaka 2013 suala lililo zua utata, lakini akajiunga na klabu ya Yanga mwaka huohuo.
Makamu wa Rais wa SC Villa Middie Nsereko ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo akisaidiwa na Ivan Kakemba kama katibu pamoja na Moses Musasizi.
Misagga amesema kuna baadhi ya watu ndani ya klabu ya Villa walikua wanaficha ukweli wa mambo wakati wa uhamisho wa baadhi ya wachezaji.
“Tumetafuta ukweli wa jinsi ulivyo. Tutamhoji kila mmoja ambaye alihusika katika na kushiriki katika miamala,” alisisitiza Misagga.
Misagga alisema, anajisikia vibaya sana kuona uongozi wao unaingia kwenye matatizo ambayo yamesababishwa na uongozi uliopita.
FIFA imewataka Villa kukamilisha uchunguzi wao kufikia tarehe 25 February. Misagga amesema kamati ni lazima iwasilishe matokeo ya utafiti wao kwa uongozi ifikapo tarehe 15 February
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni