MANCHESTER United inachuana na Sunderland katika mechi ya ligi kuu England inayopigwa uwanja wa Old Trafford jioni ya leo.
Cha kushangaza kuelekea katika mechi hiyo, Louis van Gaal amekiri kuwa timu hiyo haina mshambuliaji wa kati mpaka sasa.
Mechi
ya leo itatoa sura kama Man United wataingia UEFA msimu ujao na kama
Van Gaal ataanza kufuzu ligi ya mabingwa katika msimu wake wa kwanza
yatakuwa mafanikio makubwa kwa klabu.
Van Gaal anaamini washambuliaji wake watatu, Radamel Falcao, Wayne Rooney na Robin van Persie hawajafikia kiwango kinachotakiwa msimu huu.
Kocha
huyo wa United amesema: "Siwezi kukataa, Robin van Persia hawezi
kukataa, Falcao hawezi kukataa na Rooney hachezi sana nafasi hiyo,
lakini hatuwezi kukaa kuwa kwa sasa hatuna mshambuliaji ambaye atafunga
magoli 20 kwa msimu"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni