JOSE
ameanzisha tena vita ya maneno na chama cha soka England, FA kufuatia
kudai kuwa kempeni dhidi yake ya kuhakikisha hachukui ubingwa msimu huu
inaendelea na kweli itawagharimu Chelsea katika mbio za ubingwa.
Mourinho
ameyasema hayo baada ya kutoka sare ya 1-1 na Burnley jana Stamford
Bridge ambapo amelaumu maamuzi ya mwamuzi Martin Alkinson.
Alkinson
alimuonesha kadi nyekundu kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic na atakosa
mechi ya jumamosi ya fainali ya kombe la ligi dhidi ya Tottenham baada
ya kadi nyekundu ya dakika ya 69.
Mourinho
anadai Ashley Barnes alitakiwa kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa
kumchezea vibaya Martic na kulikosababisha kiungo wake amsukume
mshambuliaji huyo wa Burnley na kuambulia kadi nyekundu.
Pia alitakiwa kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kitendo cha kumsukuma Branislav Ivanovic.
Mourinho
anaamini haki haikutendeka ambapo walinyimwa penalti mbili kwani
Michael Kightly aliunawa mpira wa shuti la Ivanovic katika dakika ya 33'
na nahodha wa Burnley Jason Shackell alimsukuma Diego Costa eneo la
hatari dakika chache kabla ya mapumziko
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni