KATIKA habari za tetesi
za usajili ambazo zimepamba vichwa vya habari vya magazeti na mitandao
mbalimbali Ulaya ni pamoja na winga wa klabu ya Wolfsburg Kevin De
Bruyne mwenye umri wa miaka 23 kukubali kurejea katika Ligi Kuu nchini
Uingereza. Taarifa hizo zinaweza kuwa njema kwa manchester United ambao
wako tayari kutoa kitita cha paundi milioni 30 kwa ajili ya kumsajili
nyota huyo wa zamani wa Chelsea. Klabu za Liverpool na Manchester United
zimeonyesha nia baada ya kugundua kuwa beki Danilo mwenye umri wa miaka
23 amekataa kusaini mkataba mpya na FC Porto. Klabu ya Tottenham
Hotspurs inataka kumsajili beki wa Monaco Aymen Abdennour mwenye umri wa
miaka 25 huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Tunisia alionyesha nia ya
kukubali uhamisho huo. Kiungo wa Manchester United Andreas Pereira
mwenye umri wa miaka 19, anaweza kuhamia Juventus baada ya nyota huyo wa
kimataifa wa Brazil kukataa kusaini mkataba mpya. Winga wa klabu ya
Tottenham hotspurs Aaron Lennon mwenye umri wa miaka 27 amepania kusaini
mkataba wao wa kudumu na Everton anapochezea kwa mkopo huku klabu hiyo
ikiwa tayari kutoa kitita cha paundi milioni saba.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Alhamisi, 26 Februari 2015
Home
/
Unlabelled
/
TETESI ZA USAJILI ULAYA: MAN UNITED YATENGA PAUNDI MILIONI 30 KWA AJILI YA WINGA WA WOLFSBURG, LIVERPOOL, UNITED WAKABANA KOO KWA DANILO.
TETESI ZA USAJILI ULAYA: MAN UNITED YATENGA PAUNDI MILIONI 30 KWA AJILI YA WINGA WA WOLFSBURG, LIVERPOOL, UNITED WAKABANA KOO KWA DANILO.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni