JAMANI!
Arsenal 'Bai Bai' ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kutupwa nje
kwa wastani wa mabao 3-3, lakini bao la ugenini walilovuna Monaco mjini
London limewapeleka mbele.
Usiku
huu, Arsenal wameshinda mabao 2-0 dhidi ya Monaco katika mechi ya
marudiano ya hatua ya 16 ya ligi ya mabingwa, mabao yakifungwa na
Olivier Giroud dakika ya 36' na Aaron Ramsey dakika ya 79'.
Mechi ya kwanza uwanja wa Emirates Arsenal walifungwa 3-1.
Licha ya kutolewa, Arsenal wameonesha kandanda safi na kwa dakika 90 wamemiliki mpira kwa asilimia 62 kwa 38.
Pia walifanikiwa kupiga mashuti 8 yaliyolenga lango, wakati Monaco hawakupiga shuti lolote.
Arsenal ni timu ya pili ya Uingereza kutolewa ligi ya mabingwa na walianza Chelsea.
Mechi ya kwanza ugenini, Chelsea walitoka 1-1 na PSG na mechi ya pili wakatoka sare ya 2-2.
Ingawa
wastani ulikuwa 3-3, mabao mawili ya ugenini dhidi ya moja la Chelsea
la ugenini, yakawavusha PSG robo fainali ya UEFA msimu huu.
Sasa
matumaini ya Waingereza yamebakiwa kwa Manchester City ambao leo
jumatano wanakabiliana na FC Barcelona katika mchezo wa marudiano uwanja
wa Camp Nou.
Mechi ya kwanza Etihad, City walichapwa 2-1 na wahaitaji ushindi wa mabao 2-0 ili kusonga mbele moja kwa moja.
Wakishinda 1-0 watatolewa kwa goli la ugenini kwani tayari Barca walishafunga mawili ugenini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni