Bondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka, aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kutakiwa kulipa fidia ya fedha kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake amebadilishiwa adhabu ya kifungo na sasa amechiwa na kutumikia kifungo cha nje.
Cheka, alihukumiwa na Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Said Msuya, baada ya kumkuta na hatia ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake iitwayo Vijana Social iliyopo Morogoro Mjini, aitwaye Bahati Kabanda ‘Masika’.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni