Baada
ya kikosi cha Manchester United kutolewa katika michuano ya kombe la FA
kwa kipigo cha 2-1 kutoka kwa Arsenal jumatatu iliyopita, kocha wa
klabu hiyo Louis Van Gaal amesema nguvu zake zote anazielekeza katika
ligi kuu ili aweze kupata nafasi ya kucheza michuano ya klabu bingwa
msimu ujao.
Kocha
huyo amesema kikosi chake hakina uwezo wa kushinda kombe lolote msimu
huu baada ya kutolewa katika kombe la FA hivyo wakimaliza katika nafasi
ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu itakuwa ni kama wameshinda kombe
kutokana na ushindani uliopo kunako ligi hiyo "Nilipenda tucheze nusu
fainali katika kombe la FA lakini tumetolewa, hivyo nafasi iliyobaki ni
kuwania kumaliza katika nafasi nne za juu na hii itakuwa kama tumeshinda
kombe msimu huu " alisema Van Gaal.
Manchester
United imeibuka na ushindi wa 3-0 katika mechi ya jana waliyocheza
dhidi ya Tottenham Hotspurs kwenye dimba la Old Trafford na mechi ijayo
wanakibarua kizito dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni