STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 3 Machi 2015

Yanga yagomea Bodi ya ligi kuahirisha mechi yake, wasema kesho wataingiza timu uwanjani


Afisa hHabari wa klabu ya Yanga Jerry Muro amesema kesho watapeleka timu uwanjani kucheza na JKT Ruvu
Afisa Habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro amesema kesho watapeleka timu uwanjani kucheza na JKT Ruvu
Klabu ya Yanga imepinga maamuzi ya Bodi ya ligi ya kusogeza mbele mchezo kati ya Yanga na JKT Ruvu, mchezo huo awali ulikua umepangwa kufanyika Machi 4 sku ya Jumatano (kesho) kwenye uwanja wa Taifa umeahirishwa mpaka Machi 11 mwaka huu.
Yanga imelalamikia uamuzi huo kutokana na Bodi ya ligi kushindwa kukaa ikazungumza nao ila imejichukulia maamuzi tu na kupeleka mbele mchezo huo hadi Machi 11 ikiwa ni siku tatu tu kabla ya Yanga kuivaa FC Platinum ya Zimbabwe.
Msemaji wa Yanga Jerry Muro amesema, wao kesho watapeleka timu uwanjani na kama mechi haitakuwepo, na wao hawatapeleka timu uwanjani Machi 11.
“Bodi ya ligi inapaswa kuwa wazi kuhusiana na mabadiliko, sisi tuko tayari kucheza kesho, lakini si Machi 11, amesema Muro.
“Angalia baada ya hiyo mechi iliyopelekwa Machi, siku tatu mbele tutakua na mechi ya kimataifa ambapo Yanga itacheza mechi ya kombe la shirikisho na FC Platinum, alafu TFF inataka tucheze mechi ya ligi. Kwa nini kesho tusicheze na JKT Ruvu halafu baada ya siku tatu tucheze na Simba?,” Muro alihoji.
“Baada ya hapo, tutapata nafasi ya maandalizi ya wiki moja kujiandaa na mechi ya kimataifa ambayo ni muhimu zaidi,” alisema Muro
Hii ni mara ya pili Yanga inaingia kwenye mgogoro na TFF kutokana na ratiba ya ligi kuu kuingiliana na michuano ya kimataifa ya klabu hiyo, awali Yanga waliiomba TFF kusogeza mbele ratiba ya mchezo wao na Mtibwa Sugar ili wapate muda wa kujiandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya BDF XI lakini TFF ilitupilia mbali ombi hilo na kuitaka Yanga icheze mechi yake na Mtibwa kama ratiba inavyoelekeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox