Man City si mabingwa wa England. Hii ni baada
ya ushindi wa mabao 3-1 ilioupata Chelsea dhidi ya Leicester City, leo.
Ushindi huo umeiwezesha kufikisha pointi 80
wakati waliokuwa mabingwa watetezi, Man City wana pointi 67 na wakashinda mechi
zao tatu zilizobaki watafikisha pointi 79.
Sasa Chelsea iliyobakiza mechi nne mkononi,
inaendelea kushindana na Arsenal ambayo iwapo itashinda mechi zilizobaki
itafikisha pointi 82.
Hivyo Chelsea inahitaji ushindi wa mechi moja
tu kujihakikishia ubingwa.
Katika mechi ya leo, Leicester ndiyo
waliotangulia kufunga bao katika dakika ya 45.
Lakini Chelsea wakasawazisha kupitia Didier
Drogba katika dakika ya 47, John Terry akaongeza la pili kabla ya Ramirez
kufunga la tatu kwa shuti kali baada ya kutengewa na Cesc Fabregas katika
dakika ya 83.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni