Rodriguez akishangilia goli lake
Timu
ya Real Madrid imezidi kuipumulia kwa ukaribu na kuongeza presha kwa
viongozi wa ligi kuu ya Hispania timu ya Barcelona baada ya kushinda
goli 3-0 dhidi ya Almeria. Magoli ya Madrid yamefungwa na James
Rodriguez dakika ya 45 likafuatiwa na goli la kujifunga la mchezaji wa
Almeria Santos dakika ya 49 kabla ya Arbeloa kuhitimisha idadi hiyo ya
magoli dakika ya 84.
Tumeshuhudia
mbinu na matukio mengi sana yakitokea katika mpira wa miguu lakini hili
lililotokea katika mechi kati ya Real Madrid dhidi ya Almeria ni baba
lao.
Usiku
huu katika mechi iliyowakutanisha vijana wa Carlo Ancelott Real Madrid
na Almeria hasa pale mpira ulipotoka na kutakiwa kurushwa ndipo mlinzi
kwa kushoto Fabio Contreao na James Rodriguez wote walipochukua mipira
na kuirusha pamoja uwanjani kwa wakati mmoja tena kwa ustadi mkubwa,
Hii ni mara ya kwanza Dunia kushuhudia mipira miwili ikirushwa kwa pamoja uwanjani wakati mchezo ukiendelea.
MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZILIZOMALIZIKA
FT
FT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni