SIMBA
SC inamtumia kiungo wake mshambuliaji Emmanuel Okwi katika mechi ya leo
ya ligi kuu soka Tanzania bara inayopigwa uwanja wa Taifa Dar es
salaam dhidi ya Mgambo JKT.
Mechi ya kwanza iliyopigwa Mkwakwani, Mgambo walishinda magoli 2-0.
Simba
wanaingia uwanjani wakiwa na machungu ya kuchapwa 2-0 na Mbeya City
katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa mwishoni mwa juma lililopita uwanja
wa Sokoine, Mjini Mbeya.
Kuelekea
katika mpambano huo, Okwi aliyeikosa mechi iliyopita kwa kuwa na kadi
tatu za njano amesema atajitahidi kuisaidia timu yake ipate matokeo.
"Namshukuru
Mungu tuko salama, mimi na wachezaji wenzangu tuko katika morali kubwa.
Tulipoteza mechi Mbeya, hatujakata tamaa, leo tunapambana kupata pointi
tatu". Amesema Okwi.
Wakati
Okwi akiwa na matarajio ya kupata ushindi, naye mshambuliaji nyota wa
Mgambo JKT, Malimi Busungu ambeya anawaniwa na Simba, Yanga amesema leo
ni siku nyingine ya kuonesha uwezo wangu.
"Hii
ni mechi yangu muhimu kuwaonesha tena watanzania uwezo wangu,
nitapambana na kuhakikisha nakuwa chachu ya ushindi, cha msingi dhuluma
isiwepo, mechi hizi za mwisho zina mambo yake".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni