YANGA SC imeshinda magoli 3-2 dhidi ya Stand United katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa jana uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Magoli ya Yanga yalifungwa na Amissi Tambwe, Mrisho Ngassa na Saimon Msuva kwa mkwaju wa penalti.
Baada
ya kufunga goli lake, Mrisho Ngassa hakushangilia kwa kawaida yake ya
kwenda kwenye kona ya kibendera, bali alionekana akibusu mkono wake.
ALIPOULIZWA KWANINI ALIFANYA HIVYO, NGASA AKAFUNGUKA
"Nimebusu
mkono kwasabababu nimemchora 'Tattoo' mke wangu, mke wangu ndio kila
kitu, ndio mshauri wangu wa kila kitu, kwahiyo nikifunga goli lazima
nimbusu"
Tattoo niliyochora ni jina la mke wangu kwasababu nina mapenzo ya dhati kwake, yeye ndiye mshauri wangu, anaitwa Nish Radhia"
"Kuna tattoo nyingine ambayo ni siri yangu pamoja na yeye, imechorwa kifuani"
TATTOO YENYEWE HII HAPA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni