Adidas
imempa nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard viatu maalum ambavyo atavitumia
wakati wa kuwaaga mashabiki wa timu hiyo.
Viatu
hivyo atavivaa katika mechi zake mbili zilizobaki za Liverpool akianza na ile
ya Jumamosi dhidi ya Crystal Palace ambayo ni muhimu sana kwa kuwa ndiyo ya
mwisho kwake katika Uwanja wa Anfield.
Baada
ya mechi hiyo, Gerrard atavivaa tena viatu vya aina hiyo katika mechi yake ya
mwisho kabisa akiwa na Liverpool ambayo watacheza dhidi ya Stoke City wakiwa ugenini.
Gerrard
anaondoka Liverpool na kwenda kujiunga na LA Galaxy ya Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni