Mshambuliaji
asiyeisha vituko wa Liverpool, Mario Balotelli ametozwa faini ya pauni 800
pamoja na kufungiwa kuendesha gari kwa siku 28.
Balotelli amekutana
na adhabu hiyo baada ya kubainika aliendesha gari kwa kasi ya maili 109 kwa
saa. Sheria ikafuata mkondo wake kupitia wahusika nchini England.
Muitaliano huyo alifanya hivyo na alipokamatwa akakubali kosa hilo wakati akiendesha gari lake la kifahari aina ya Ferrari lenye thamani ya pauni 240,000.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni