STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 16 Mei 2015

KWA TAARIFA YAKO; HUYU NDIYE STEVEN GERRARD

Na Mr Choi
Mnamo tarehe 30 mwezi wa tano miaka ya 1980 kwenye kijiji cha Whiston Merseyside jijini Liverpool ndipo alipo zaliwa mzalendo wa kweli Mfalme miongoni mwa Wafalme katika timu ya Liverpool namzungumzia mwana wa George Gerrard si mwingine ni Steven. 
 
Hapa nakwenda kukujuza yanayo muhusu kiongozi tena muhamasishaji mwenye uzalendo halisia si mwingine ni Steven Gerrard alie anza maisha yake ya soka kwenye timu ya kitaa Whiston Juniour kama ilivyo kwa baadhi ya timu zetu za mitaani. 

Waswahili husema kizuri kinajiuza na kibaya kinajitembeza aaa hiyo ni misemo yenye uhalisia kwani akiwa na timu hiyo ya kitaa moja ya watafuta vipaji wa timu ya Liverpool ( Scout ) kwenye pitapita zake maeneo ya Whiston ndipo akamuona kinda alie kuwa na miaka 7 aki kinukisha kweli, kiukweli hakufanya makosa alifanya mchakato wa haraka na kuhakikisha kinda huyo anatimba kwenye shule ya vipaji ya Liverpool na hilo lilitimia mwaka 1987. 

Kizuri ni kizuri na panapo juhudi sikufichi mafanikio huonekana mapema akiwa kwenye shule ya vijogoo juhudi zake zilionekana mpaka kupelekea Mashetani wekundu wa Manchester kuwa na matamanio hapo alikuwa na miaka 14 wanasema "Ngastuka na Machale Kuncheza" chale zikacheza kwa uongozi wa Liverpool ikabidi wamsainishe mkataba wa chipukizi (YTS) na ndo ikawa pona yao kuto kumpoteza mwana wa George. 

Akiwa na miaka 14-17 alicheza takribani michezo 20 na ilipo fika tarehe 5 mwezi wa 11 mwaka 1997 ndipo nuru na mwangaza wa taswira ya Gerrard ikaonekana kwani alisaini mkataba kama mchezaji wa kulipwa viunga vya Anfield. 

Baada ya kusaini mkataba ule mwangaza ukazidi kumuangazia kwani tarehe 29/11/1998 akiwa na miaka 18 akacheza mchezo wake wa kwanza ktk kikosi cha kwanza aki ingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Vegard Heggem kwenye mchezo dhidi ya Blackburn na Liver ili ibuka na ushindi wa 2-0 hapohapo msimu wa 98/99 alicheza mchezo wake wa kwanza ktk mashindano ya Uefa ilikuwa dhidi ya Celta Vigo Uefa Cup akichukua nafasi ya mtaalamu Jamie Redknapp aliepata majeraha na msimu huo alicheza michezo 13. 

Msimu wa 1999/00 yakajitokeza matukio mawili makubwa kwenye historia ya mchezaji huyu tukio la kwanza alifunga goli lake la kwanza ulikuwa mchezo dhidi ya Sheffield Wednesday aaa hapo jamaa alishangilia balaaa hapo alikuwa moto si unajua harakati za kutafuta namba ukiachilia tukio la goli kingine ni mchezo dhidi ya Everton akiingia kuchukua nafasi ya Robbie Fowler dakika ya (66 ) ambapo alioneshwa kadi nyekundu ya kwanza kwa kumchezea faulo Kevin Campbell dakika ya (90) hiyo ilikuwa ni sawa na kupasuka ngoma kwenye ngoma ya watani wa jadi. 

Katika msimu huo na muendelezo wa kiwango bora kabisa kocha wa kipindi hicho Mzee Gerrard Houllier ndipo akazidi ng'arisha nyota ya Steven kwa kumuanzisha ktk baadhi ya michezo huku takribani michezo 6 Gerrard akicheza pamoja na kiungo mtata enzi hizo Jamie Redknapp. 

Nadhani kila mtu, kila kona ya mdau wa soka uki muuliza juu ya wachezaji wa ligi ya Uingereza wenye michomo ( mashuti) hususani katika kariba ya ubora wao huwezi muacha Gerrard na moja ya magoli murua ya jembe hili ni msimu wa 2000/01 takribani yard 25 akiwafunga United pale Anfield ni mchezaji ambae hupaswi kumuacha huru akiwa na mpira nje ya 18 na ndani kwani kitakacho tokea kama si nyavu kucheka basi utamuuliza kipa shughuli ya kuokoa mashuti yake na ndo mwanzo mzuri ukaanza kwa kupata nafasi ya kucheza kwa wingi. 

Msimu huohuo alifunga goli lake la kwanza mashindano ya Uefa kwenye fainal ya Uefa cup dhidi ya Alaves kwa timu yake ya Liver kuibuka na ushindi wa magoli 5-4 . Pia ndani ya msimu huo 2001 alitwaa tuzo ya chipukizi bora wa ligi kuu Uingeraza tuzo zinazotolewa na chama cha wachezaji wa kulipwa (PFA). 

 Mwezi wa kumi 2003 kocha Gerrard Houllier akufanya makosa kwa kumtangaza Steven Gerrard kuchukua nafasi ya Sami Hyypia kuwa nahodha wa kikosi cha Majogoo wa Anfield unajua wapo wanao sifiwa pasipo kuona sifa wanazo pewa ila iko wazi hakuna anaepinga uthibitisho wa ubora wa Gerrard hata wale walio kutana nae ndani ya dimba hawa achi kusimulia shughuli pevu ya mwana wa George na kupewa kwake unahodha alisha thibitisha ustahili wake. 

Nadhani unatambua si kila Mjamaa ana uhalisia wa Ujamaa na kufuata misingi yake hiko kipo hadharani upo wapi Ujamaa wa Nyerere na huwezi kujiita mzalendo kwa misingi ya kuiga maisha tuache hayo lakini maana yangu kubwa ni kukujuza juu ya Uzalendo halisia wa Gerrard kwa timu yake ya Liverpool Msimu wa 2003/04 kuondoka kwa Gerrard Houllier kukaleta kimsuguano kwa wana wa Anfield kitu kilicho pelekea Chelsea ambayo ilikuwa inamwaga mapesa ya Abramovich kutaka kumsajili Gerrard lakini mzalendo ni mzalendo kitita cha paundi millioni 20 kiligonga mwamba kwa mchezaji huyo kuthibitisha ata dumu Anfield. 

Mnamo tarehe 25/5/2005 ni siku ambayo kila mwanamichezo ulimwenguni kote alistaajabu si yale ya Musa ya kale hapana bali ni Liverpool kutwaa ubingwa wa Uefa katika upekee wa kipekee viunga vya Instabul-Uturuki kwenye dimba la Ataturk watazamaji 68,600 na Dunia ya michezo waki amini Ac Milan wametwaa ndoo kwani mpaka mapumziko walikuwa wanaongoza 3-0 ila kipindi cha pili kibao kiligeuka kwa Liver kusawazisha magoli yote matatu Gerrard akiwa moja ya watupiaji kisha timu yake kutwaa ubingwa kwa jumla ya penalti 3-2.

Hapo ndipo tukaona nini maana ya nahodha ktk timu na yapi majukumu yake Gerrard alionesha ulimwengu kiukweli na andika huku niki sisimuka kwa hisia za fainal hii kwa hamasa na upambanaji wa Gerrard mchezaji ambae anauwezo wa kucheza sehemu tatu kuu kiungo wa chini,juu na mshambuliaji wa pili. 

Yapo mengi na matamu ya mzalendo huyo alieshawishiwa na vilabu kadha wa kadha kuikacha Liver ila alibaki na dhamira yake msimu wa 2005/06 alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi kuu PFA na hii ikawa baada ya miaka kadhaa kwa mchezaji wa Liverpool kutwaa (1988-John Barnes). Msimu wa 2008/09 mwezi wa tatu tukashuhudia hatrick yake ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa safari ni ndefu kweli maana kila kona naona ukali wa mkongwe huyu anae ikacha ligi kuu ya Uingereza msimu huu wa 2014-2015. 

Ni miongoni mwa wachezaji wachache pale Anfield kucheza michezo zaidi ya 500 huku kwenye timu ya Taifa ambapo alikuwa nahodha 2010 aki bahatika kucheza michezo 114 ambayo imemuwezesha kushika nafasi ya tatu kwenye listi ya wachezaji walio cheza michezo mingi timu ya Taifa ( Peter Shilton-125,Beckam-115,Gerrard-114) huku akipachika magoli 21 alistaafu timu ya Taifa 2014 baada ya kombe la Dunia mwezi wa saba na kumbuka kacheza kombe la Dunia mara tatu (2006/2010/2014). 

Kila mtu lazima ashangae kwani magwiji wanao ondoka msimu ligi kuu Uingereza ni wawili Gerrard na Lampard kwa nini Steven ndo amekuwa gumzo kubwa kila kona tofauti na Lampard aliefanya makubwa pia hata na wengine waliopita jibu ni moja tu faida na matunda ya Ujamaa/ Uzalendo ndo haya staki nikupeleke kwa kina Mao Tse-tung ila jamaa alionesha dhamira na alijitoa kupambana pale Anfield bila kuchoka wala kuikacha timu hiyo. 

Maisha yake Anfield ukiachilia tuzo mbalimbali alizo pata upande wa vikombe kasha chukua KOMBE LA LIGI-3 KOMBE LA FA-2 UEFA SUPER CUP-2 MABIGWA UEFA -1 UEFA CUP-1 Ni kombe la Ligi kuu ndilo ambalo ajachukua miongoni mwa makombe makubwa ngazi ya vilabu na ndicho kitu kinacho muuma mpaka sasa msimu 2013-14 alimanusura Liverpool ichukue ubingwa lakini harakati zilifikia tamati ktk moja ya michezo ambayo mchezaji huyu hata sahau katika maisha yake ilikuwa dhidi ya Chelsea kwa timu yake kufungwa 1-0 goli la Demba Ba alie utwaa mpira kutoka kwa Gerrard kila mtu hakuamini kilicho tokea kwa Mfalme kuanguka kwenye vita vikali adui akimpokonya silaha kiukweli ilikuwa dhahma na Jahazi likazama. 

Wengi wakasema umri, kiwango kimeshuka sawa yawezekana ingawa nikamtizama mkongwe Pirlo anavyo kinukisha hivi sasa nika kumbuka athari za kutumika mno akiwa bado mdogo sikusahau kuangazia kudungwa nganzi pia hapo- hapo kwa Pirlo nika tizama maisha ya wachezaji wa Italy wanavyo dumu kwa muda mrefu dimbani kulinganisha na Uingereza ila mwisho wa siku hakuna kilicho na mwanzo kukosa mwisho mchezo wao dhidi ya C.Palace viunga vya Anfield ndipo sherehe kubwa itafanyika ya kumuaga rasmi gwiji/ mzalendo huyu alie kipiga zaidi ya miaka 20 viunga vya Anfield shamrashamra na majonzi vimetawala. For more/ Ushauri:: Choikangta.ckt@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox