Ni
kawaida kwa kila bingwa wa ligi kuu England kuwa na namna yake ya
kusherekea ubingwa wake, hivyo Chelsea nao wapo katika mipango madhubuti
ya kufanya tukio hilo kubwa.
Klabu na wasimamizi wa ligi wanakaa chini na kupanga sherehe za ubingwa ambazo zitajumuisha wachezaji watakaopewa medali.
Kama
unavyojua kwa Chelsea, kuna wachezaji walikuja katikati ya msimu na
wengine waliondoka, hivyo klabu inatakiwa kupiga hesabu ni wachezaji
gani wana sifa ya kuvaa medali na ambao hawatavaa.
Mchezaji
angalau anatakiwa kuanza kikosi cha kwanza katika mechi tano (5) za
ligi kuu ili kukidhi kigezo cha kuvaa medali-kwahiyo Fernando Torres
amekosa sifa kwasababu alianza mechi moja tu kabla ya kupelekwa kwa
mkopo mwezi wa nane mwaka jana.
Andre
Schurrle aliuzwa katika klabu ya Wolfsburg wakati wa dirisha dogo la
mwezi januari mwaka huu, lakini alianza mechi 9 katika nusu msimu
alioichezea Chelsea, hivyo Mjerumani huyo ana vigezo vya kuvaa medali.
Akihojiana na John Bennett wa BBC, nyota huyo tayari amethibitisha kuwa Jose Mourinho amemtaarifu kurudi London kuvaa medali.
Some ujumbe huu hapa chini;
"Jose text me to tell me I've got a medal." Hear some of my interview with@Andre_Schuerrle on @wsworldfootball. #CFCpic.twitter.com/oWwKVTokRn
— John Bennett (@JohnBennettBBC) May 14, 2015
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni